Waasi waliokuwa na silaha wamewaua watu 15 katika jimbo la Ituri mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, duru za ndani zilisema Jumapili, katika shambulio la pili la aina hiyo ndani ya siku chache.
Vyanzo hivyo vilisema wanamgambo wa CODECO (Ushirika wa Maendeleo ya Kongo), ambao wanadai kutetea masilahi ya kabila la Lendu, walilenga tena watu kutoka kabila hasimu la Hema.
Wapiganaji wa CODECO waliwavizia watumiaji wa barabara karibu na kijiji cha Tali ambapo waliwasimamisha watu 15, akiwemo mwanamke mmoja, Jumamosi mchana, alisema Jules Tsuba, kiongozi wa mashirika ya kiraia huko Djugu, mji wa eneo hilo.
Wanamgambo hao waliwafunga na kuwavua nguo kabla ya kuwaua huku baadhi ya wahasiriwa “walikatwa koo, wengine walipigwa risasi na kufa”, alisema.
Kulingana na chanzo cha kibinadamu, “miili ya wahasiriwa ina alama za mateso”.