Kylian Mbappe amekubali mkataba wa miaka mitano na Real Madrid, kwa mujibu wa Marca.
Fowadi huyo wa Ufaransa, ambaye mkataba wake na Paris Saint-Germain unamalizika mwishoni mwa msimu huu, atajiunga na Madrid mnamo Julai 1.
Kwa mujibu wa gazeti la Uhispania, Mbappe alisaini mkataba na Madrid wiki mbili zilizopita.
Wakati huo huo, Rais wa LaLiga Javier Tebas anasema angekaribisha ujio wa Mbappe Real Madrid.
“Mwaka huu sisi (LaLiga) tuna mchezaji bora zaidi duniani ambaye ni (Jude wa Real Madrid) Bellingham,” Tebas alisema.
“Msimu uliopita (Robert wa Barcelona) Lewandowski alicheza kwa kiwango cha juu. Atletico ina (Antoine) Griezmann na iwapo (Kylian) Mbappe atawasili, hiyo itatusaidia (LaLiga) kuwa na ushindani zaidi na kukua kwa kasi zaidi.”