Mtu mmoja amefariki na wengine saba kujeruhiwa katika ajali iliyohusisha gari la abiria aina ya Tata yenye namba za usajili T 596 EAF inayofanya safari zake Morogoro _Mlimba kugongana uso Kwa uso na bajaji iliyokuwa inatokea Mindu kuelekea Morogoro Mjini.
Mmoja wa Majeruhi hao Angel Zacharia amesema ajali hiyo imetokea katika eneo la Mindu Barabara kuu ya Morogoro _Iringa majira ya asubuhi moja asubuhi huku chanzo chake kikiwa ni uzembe wa dereva wa basi la abiria kuhama upande wake bila kuchukua tahadhari na kuigonga bajaji hiyo
Daktari Kutoka kitengo Cha dharula hospital ya Rufaa Mkoa Morogoro Joseph Kwai amekiri kupokea mwili wa marehemu ambaye ni mwanamke aliyekuwa abiria wa bajaji huku majeruhi hao wakitokea kwenye basi na bajaji.