Mwanaume mmoja raia wa Uholanzi alitozwa faini ya euro 380 ($400) baada ya kamera inayotumia AI kumnasa akizungumza kwenye simu yake akiendesha gari huku yeue akidai alikuwa anakuna kichwa tu na mfumo ukafanya makosa kuipiga picha yake.
Mnamo Novemba mwaka jana, Tim Hansen alipokea faini kwa madai ya kuzungumza na simu yake ya mkononi wakati akiendesha gari mwezi mmoja uliopita.
Alishtuka, haswa kwa sababu hakukumbuka kutumia simu yake kwenye siku hiyo, kwa hivyo aliamua kuangalia picha iliyonaswa Mahakamani.\
Kwa mtazamo wa kwanza ilisemekana kuwa inaonekana kwamba Tim anazungumza kwa kweli kwenye simu yake, lakini uchunguzi wa karibu unaonyesha kwamba hakuwa ameshikilia chochote mkononi mwake na alikuwa akikuna tu upande wa kichwa chake na kamera ikakosea msimamo wa mkono wake kwa kushika simu.