Jeshi nchini Myanmar limewahukumu kifo mabrigedia jenerali watatu waliojisalimisha pamoja na mamia ya wanajeshi na kukabidhi mji wa kimkakati kwenye mpaka wa China kwa makundi ya waasi mwezi January.
Chanzo cha kijeshi kilisema kuwa maafisa watatu wakuu wa kijeshi, akiwemo kamanda wa mji wa Laukkai. walipewa hukumu ya kifo, liliripoti shirika la habari la AFP siku ya Jumatatu (Feb 19).
Bado haijafahamika ni lini hukumu hii ilitolewa. Hapo awali, msemaji wa jeshi aliambia shirika la habari kwamba majenerali wa Brigedia walikuwa chini ya ulinzi wa kijeshi.
Wakati huo huo, majenerali wengine watatu wa Brigedia walihukumiwa kifungo cha maisha kwa jukumu lao katika kujisalimisha.
Mnamo Januari, mamia ya wanajeshi walijisalimisha huko Laukkai kaskazini mwa jimbo la Shan kwa Muungano wa Udugu Watatu kufuatia mapigano ya miezi kadhaa na kujisalimisha huku ilikuwa moja ya hasara kubwa kwa jeshi katika miongo kadhaa. Ilizua ukosoaji wa nadra wa junta na wafuasi wake.