Mtandao wa kijamii wa X, ambao zamani ulijulikana kama Twitter, unaendelea kutoweza kufikiwa na watumiaji nchini Pakistan baada ya vikundi vya waangalizi wa mtandao kuanza kuripoti kukatika kwa mtandao siku ya Jumamosi.
NetBlocks, shirika linalofuatilia masuala ya ufikiaji kwenye mtandao, Mnamo Februari 17 ilithibitisha kwamba “mvurugiko wa kiwango cha kitaifa” umekumba X nchini Pakistani baada ya maandamano makubwa nchini humo yaliyochochewa na madai ya wizi wa kura katika uchaguzi mkuu.
Maafisa wa serikali, hata hivyo, wamekataa kukubali taarifa za kizuizi chochote kama hicho.
Gohar Ejaz, waziri mwenye dhamana wa mambo ya ndani, aliiambia Al Jazeera kwamba hajui vikwazo vyovyote vile. “Hakuna taarifa. haiingii chini ya [wizara] ya mambo ya ndani,” aliiambia Al Jazeera kupitia ujumbe wa WhatsApp.
Maafisa katika Mamlaka ya Mawasiliano ya Pakistani (PTA), chombo cha udhibiti wa serikali, hawakujibu maswali mengi juu ya kufungwa lakini walionyesha kuwa PTA ni shirika la udhibiti ambalo linatekeleza maagizo yaliyotolewa na serikali.