Moto ambao chanzo chake bado hakijajulikana umeteketeza maduka ya Wafanyabiashara wa nafaka maeneo ya Ubungo Riverside Jijini Dar es salaam usiku huu.
Ayo TV imefika eneo la tukio na kuongea na Mashuhuda, Wafanyabiashara na Afisa wa Zimamoto Inspekta Helman Edwin ambaye amesema maduka matatu yametekea kwa moto.
“Chanzo cha moto hakijajulikana ila tunaendelea kufanya tathmini, hakuna madhara yoyote kwa Binadamu zaidi ya mali kuungua”