Katika tukio la kipekee linaloangazia ushirikiano wa biashara kati ya Tanzania na MISRI, Mkurugenzi Mkuu wa TanTrade, Bi. Latifa M. Khamis, pamoja na viongozi wengine waandamizi akiwemo Mhe.Luteni Jenerali Kamal Al- Wazir, Waziri wa Usafirishaji wa MISRI, wamekutana Dar es Salaam katika mkutano unaoashiria hatua muhimu katika kuimarishwa maslahi ya kiuchumi na uhusiano wa kitamaduni kati ya nchi hizi mbili.
Moja ya vipaombele vya Mhe. Dr. Samia Suluhu Hassan, Raisi wa Jamuhuri ya Muungano w Tanzania ni kuimarisha na kuongeza thamani ya biashara kati yao. Tanzania huuza bidhaa zanye thamani ya takriban Dola za kimarekani 4,867 kwenda Misri na huagiza bidhaa zenye thamani ya Dola za kimarekani 49,293 kutoka Misri kila mwaka.
Lengo likiwa kuongeza na kupanua biashara kati ya nchi zetu kukutana, kubadilishana maarifa na Kutafuta fursa mpya za biashara endelevu. Mwaka wa fedha 2023/2024 umeshuhudia juhudi nyingi za kusaidia biashara ndogo na za kati za Tanzania kuuza zaidi nje ya nchi nankufikia masoko mapya.
Katika kuonyesha umuhimu wa ushirikiano huu, TanTrade imekaribisha Kampuni za Misri kushiriki katika Maonyesho ya 48 ya Biashara ya Kimataifa ya Dar es salaam, Yatakayofanyika kuanzia tarehe 28 Juni hadi 13 Julai 2024. Maonyesho haya ni muhimu kwa kuonyesha teknolojia mpya na kukuza mtandao wa biashara kimataifa katika Afrika Mashariki na kati.