Ole Gunnar Solskjaer ameibuka kama mgombea wa ghafla kuchukua nafasi ya Thomas Tuchel kama meneja wa Bayern Munich.
Ripoti katika gazeti la The Sun inadai kuwa Bayern “wanafikiria kumnunua” meneja huyo wa zamani wa Manchester United, ambaye amekuwa hana kazi tangu kutimuliwa na wababe hao wa Premier League mwaka 2021.
Tuchel anasemekana kuwa chini ya shinikizo baada ya kushindwa mara tatu mfululizo, na cha hivi punde Jumapili walipochapwa 3-2 na Bochum
Ripoti hiyo inasema: “Ole Gunnar Solskjaer anapangwa kuchukua nafasi ya Thomas Tuchel huko Bayern Munich, kulingana na ripoti za kushangaza
“Tuchel anajikuta chini ya shinikizo kubwa katika Allianz Arena kufuatia kushindwa mara tatu mfululizo.
“Hilo linawaweka mabingwa watetezi wa Bundesliga katika hatari kubwa ya kutolewa mapema Ligi ya Mabingwa kwa Lazio na pointi nane kutoka kwa Bayer Leverkusen.