Chuo cha ufundi Arusha (ATC) kimehitimisha mafunzo ya ukaguzi wa magari kwa askari wa kikosi cha usalama barabarani nchini ambacho kilihusisha wakuu wa kikosi cha usalama barabarani na wakaguzi wa magari (vehicle inspectors) kote nchini ambacho kilianza februari 19 hadi 20 mwaka huu katika chuo cha ufundi Arusha.
Akiongea mara baada ya mafunzo hayo leo februari 20,2024 katika chuo cha Ufundi Arusha kamanda wa kikosi cha usalama barabarani nchini Naibu kamishna wa Polisi DCP Ramadhani Ng’anzi amesema lengo la mafunzo hayo ni kuwajengea uwezo wakaguzi wa magari ili kwendana mifumo ya kiksasa na magari ya kisasa yanayoingia nchini.
Ameongeza kuwa ifikapo mwezi machi mwaka huu kikosi hicho kitaanza kufanya ukaguzi wa magari kwa kutumia mifumo ya kisasa katika kubaini vyombo vyenye changamoto za kiundi huku akiwaomba wananchi kupokea mabadiliko hayo yanayokwenda na duniani ya sasa huku kiwapongeza chuo cha ufundi Arusha kwa namna ambavyo wanafundisha kwa kutumia vifaa vya kisasa.
Kwa upande wake Mkuu wa idara ya Uhandisi Magari kutoka chuo cha ufundi Arusha Injiania David Mtunguja amesema chuo hicho ni miongoni mwa vyuo bora Afrika katika idara ya uandishi magari ambapo amebainisha kuwa endapo wakaguzi wa magari watasoma katika chuo hicho watapata maarifa mazuri na bora katika utendaji wa kazi zao.
Nae Mkurungenzi wa udhibiti Usafiri wa Barabara kutoka Latra Bw. Johansen Kahatano amesema chuo cha ufundi Arusha kimejipanga vizuri katika maswala ya usalama barabarani huku akisema chuo hicho kinashirikiana na mamlaka ya udhibiti usafiri Ardhini (LATRA) katika kuboresha mifumo ya utambulisho ya njiani za mabasi hapa nchini.
Mkuu wa chuo cha ufundi Arusha Dkt. Musa Chacha amesema kuwa wataendelea kushirikiana na Jeshi la Polisi katika kuwajengea uwezo wakaguzi wa magari ili kuwa na ufanisi katika ukaguzi magari hapa nchini huku akimshukuru Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini kwa kuridhia wakaguzi hao kupata mafunzo chuo hapo.
Nao baadhi ya wakuu kikosi cha usalama Barabara waliohudhuria mafunzo hayo katika chuo cha ufundi Arusha Pamoja na kushuru kwa kupata mafunzo yenye viwango vya Juu na mbadiliko ya sayansia na Teknolojia wamehaidi Kwenda kuleta matokeo Chanya katika ukaguzi wa magari na kuwaelekeza askari kusimamia vyema ukaguzi huo wa magari kama walivyojifunza.