Kiwango cha matumizi ya kila mwaka cha Barcelona kimepunguzwa kwa zaidi ya €66m , kutoka €270m hadi €204m, na kulingana na jarida la The Sun linadai kuwa klabu hiyo itahitaji kuwaondoa wachezaji kadhaa msimu huu wa joto.
Frenkie de Jong, Robert Lewandowski, Gavi, Raphinha, Ronald Araujo na Pedri wote wameorodheshwa kama chaguo iwezekanavyo kwani ni miongoni mwa wale ambao wangevutia ada kubwa zaidi za uhamisho, huku pia wakiwa kwenye mishahara ya juu zaidi.
Baada ya kupunguzwa kwa €400m hapo awali mnamo Septemba, punguzo la hivi karibuni linaonyesha ukubwa wa changamoto inayowakabili Barca wanapojaribu kuwa washindani katika soko la uhamisho kwa mara nyingine tena.
Vyanzo vimeiambia ESPN kwamba gharama za kikosi — ambayo ni kiwango kinachodhibitiwa — ni zaidi ya €400m, ambayo ni zaidi ya mara mbili ya kikomo kilichowekwa na LaLiga.
Matokeo yake, klabu iko chini ya vikwazo vya kifedha.