Takriban Wapalestina 29,313 wameuawa na 69,333 kujeruhiwa katika mashambulizi ya Israel huko Gaza tangu Oktoba 7, wizara ya afya katika eneo linaloongozwa na Hamas ilisema katika taarifa yake siku ya Jumatano.
Takriban Wapalestina sita waliuawa Jumatano asubuhi kutokana na shambulio la anga la Israel kwenye gari lao katika mji wa Deir al-Balah, katikati mwa Ukanda wa Gaza.
Watu walioshuhudia tukio hilo walimwambia mwandishi wa habari wa Anadolu kwamba ndege ya kivita ya Israel iligonga gari la raia, wakati ikipita kwenye barabara ya “Abu Hosni”, katikati mwa Deir al-Balah.
Chanzo cha matibabu pia kiliiambia Anadolu kwamba shambulio la anga la Israel limesababisha vifo vya Wapalestina sita, wakiwemo watano waliokuwa kwenye gari lililolengwa na mpita njia mmoja, pamoja na idadi ya watu waliojeruhiwa.
Wakati huo huo, ripota wa Anadolu ameongeza kuwa, makombora ya Israel yamekuwa yakishambulia maeneo ya mashariki ya Deir al-Balah tangu alfajiri ya Jumatano.