Jeshi la Polisi kikosi cha usalama barabarani kimesema licha ya kuwa na dhamana ya kusimamia usalama wa barabara hapa nchini kitaendelea kuwa balozi wa utalii huku kikiwaomba wadau wa utalii kitumia wataalam wa Jeshi hilo kukagua magari yao.
Kauli hiyo imekuja baada ya kutembelea hifadhi ya Tarangire iliyopo kaskazini mwa Tanzania ambapo baadhi ya maafisa waandamizi wa kikosi hicho kutoka Makao Makuu na wakuu wa kikosi cha usalama barabarani pamoja na wakaguzi wa magari waliomaliza mafunzo yao katika chuo cha ufundi Arusha wamewaomba wadau wa utalii kuhakikisha wanakagua magari yao mara Kwa mara Ili kuviweka katika hali ya Usalama vyombo vyao.
Afisa mnadhimu wa kikosi cha usalama Barabarani kutoka Makao Makuu ya kikosi hicho kamishna msaidizi wa Polisi ACP Pili Misungwi.
Wakuu hao wa kikosi na wakaguzi Kwa pamoja wamapata fursa ya kutembelea hifadhi hiyo huku wakivutiwa na vivutio mbalimbali ambavyo vipo Tarangire ambapo wamewaomba wananchi na askari wengine wa vyombo vya ulinzi na usalama kutembelea vivutio hivyo ili kushuhudia maajabu ya dunia.
Aidha wamebainisha kuwa mafunzo waliyoyapata yatawasaidia pia sekta hiyo ya utalii ambayo inaingiza pato kubwa Kwa taifa huku ikiwataka kuwatumia wakaguzi wa magari wa Jeshi hilo ambao watambulika kisheria.
Pia kikosi hicho kimewaomba wadau wa utalii kufanya ukaguzi wa magari yao mara Kwa mara Ili kutoa huduma bora Kwa watalii wa ndani na nje ya Nchi.