Rashidi Hussein Mkayala mkazi wa mtaa Gemu kata ya Mwanga Kusini Manispaa ya Kigoma Ujiji amejinyonga kwa kutumia kilemba cha kiume cha kuvaa kichwani (Haghali) muda mfupi baada ya kumuua mke wake Bernadeta Cosmas(33) kwa kumnyonga shingo hadi kufa katika kile kinachoelezwa kutokea mgogoro baina ya wanandoa hao.
Mwenyekiti wa Mtaa Gemu,Buswalu Mulumbu Mkama akizungumzia na @ayotv_ eneo la tukio hilo amesema kuwa chanzo cha tukio hilo ni mgogoro uliotokea siku za nyuma ambapo Mke wa marehemu alifika kwa mwenyekiti na kutoa taarifa ya vitendo vya mume wake kuchukua vitu vya ndani na kuuza ambapo mara kadhaa kesi za wanandoa hao zilikuwa zikipelekwa kwake kwa ajili ya usuluhishi.
Mwenyekiti huyo alisema kuwa siku moja kabla tukio marehemu alilala nyumbani kwake baada ya kukimbia nyumbani kwa mume wake kufuatia kipigo alichopata kwa mume wake ambapo katika tukio hilo alinusurika kuuawa baada ya kukabwa shingo na waya wa umeme hivyo alipopata nafasi ya kuchomoka alikimbia na kukimbilia kwa mwenyekiti wa mtaa ambapo alilala hadi siku ya tukio ambapo kabla tukio kaka wa mareheme alipokuja kumchukua ndugu yake.
Uchunguzi wa awali wa tukio hilo unaonyesha kuwa Marehemu Rashidi Hussein alimnyonga mke wake kwa mikono hadi kumuua na baadaye kutoka nje ambapo alifunga mlango kwa nje na kurudi ndani kupitia dirishani ambapo alifunga milango yote na madirisha na yeye kujinyonga kwa kitambaa cha kichwani.
Mtoto wa marehemu, Hussein Rashidi akieleza tukio hilo alisema kuwa kumekuwa na ugomvi wa mara kwa mara wa wazazi wake usiku mmoja kabla ya tukio walilala kwa Mwenyekiti wa mtaa baada ya baba yake kumpiga mama yake na kumuumiza.
Kwa sasa miili yote miwili imehifadhiwa kwenye hospitali ya rufaa ya mkoa Kigoma maweni wakati uchunguzi wa tukio hilo ukiendelea na Jeshi la Polisi