Nyota wa soka wa Brazil, Neymar amepokea onyo kutoka kwa kocha wa timu ya taifa, Dorival Junior, kuhusiana na kurejea kwake kikosini, baada ya kusema kuwa hana uhakika wa kurejea katika timu ya taifa ya Brazil kulingana na GOAL.
Neymar amekuwa nje ya uwanja kutokana na kupasuka kwa ligament ya anterior cruciate ambayo ilihitaji kufanyiwa upasuaji Oktoba mwaka jana. Ingawa mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 32 alikuwa na matumaini ya kurejea Copa America 2024, daktari wa timu hiyo alimkataa.
Dorival alisisitiza kwamba Neymar lazima aonyeshe usawa na umakini kabla ya kuitwa kwenye timu ya taifa.
Akizungumzia suala hilo, Dorival alisema, “Yeye ni mmoja wa wachezaji wakubwa katika soka la duniani matumaini yetu ni kwamba atapona kimwili.
Ana nafasi [katika kikosi] kwa kila kitu ambacho amekamilisha katika timu ya taifa, lakini anahitaji kujiamini, utulivu, usawa, na, zaidi ya yote, kuzingatia na atakuwa sehemu ya mchakato huo mradi tu atakuwa amepona kabisa.”