Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mhe Albert Chalamila ameyasema hayo leo Februari 21,2024 alipotembelea kiwanda cha chupa za plastic zilizotumika eneo la viwanda Mikocheni Wilaya ya Kinondoni.
RC Chalamila akiwa katika muendelezo wa ziara yake ya kukagua miradi mbalimbali ya maendeleo pamoja na kusikiliza kero za wananchi katika Wilaya zote za Mkoa huo ikiwa leo ni siku ya tatu toka aanze ziara yake.
Mhe Albert Chalamila ameridhishwa na utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo katika jimbo la Kinondoni kama vile miradi ya ujenzi wa vyumba vya madarasa, na kituo cha afya.
Aidha RC Chalamila amesema ni wakati muafaka kila mwananchi akitazama taka imjie fedha, imjie Ajira, imjie Nishati pia imjie namna bora ya kuweka jiji safi
Kwa kuwa jiji la Dar es Salaam lina kua kwa kasi sana ambapo linakadiriwa ifikapo 2030 litakuwa miongoni mwa majiji makubwa kati ya majiji 7 ya Afrika, hivyo ni vema kujipanga katika usafi vilevile upangaji mzuri wa miji yetu kwa kuwa haiwezekani kuwa Mega City wakati ni chafu na halijapangika.
Vilevile RC Chalamila amemtaka mwekezaji wa kiwanda cha chupa za plastic zilizotumika kufungua njia mara moja ambayo inalalamikiwa imezibwa kutokana na kulundika malighafi zake za chupa.
Naye Mkurugenzi wa Manispaa ya Kinondoni Bi Hanifa amesema Manispaa hiyo imeshatenga maeneo makubwa ya kuweza kuwekeza viwanda vya namna hiyo eneo la Mabwepande hivyo kila mtu ruksa kuomba.
Mwisho RC Chalamila amesema viwanda vya aina hiyo ni muhimu Katika jiji kwa kuwa husaidia kuliweka jiji safi wakati wote na kujikinga na magonjwa ya milipuko, wakati ni sasa tubadili fikra vilevile RC Chalamila anatarajia kuendelea na ziara yake katika Wilaya hiyo kesho Februari 22,2024 Jimbo la Kawe.