Shirika la umoja wa Mataifa la mpango wa chakula WFP, linasema miezi kumi tangu kuzuka kwa vita nchini Sudan, maelfu ya raia wa nchi hiyo hawana chakula.Shirika la umoja wa Mataifa la mpango wa chakula WFP, linasema miezi kumi tangu kuzuka kwa vita nchini Sudan, maelfu ya raia wa nchi hiyo hawana chakula.
Kwa mujibu wa WFP, wakati huu, chini ya asilimia tano ya raia wa Sudan wanaweza kumudu mlo mmoja pekee, alisema Eddie Rowe, mkuu wa shirika hilo nchini Sudan, alipozungumza na waandishi wa habari mjini Brussels.
WFP inasema inakabiliwa na ukata huku ikilazimika kusitisha baadhi ya operesheni zake za ugawaji wa chakula kutokana na usalama mdogo kwenye baadhi ya maeneo, ambapo umesababisha raia kushindwa kufanya kilimo cha kujikimu.
Kwa miezi kadhaa sasa Mashirika ya misaada yameonya kuhusu kukwama kwa upatikanaji wa misaada ya kibinadamu na ufadhili mdogo wa fedha, hali inayotishia kushuhidiwa kwa baa la njaa kwenye taifa hilo.