Waziri wa Kilimo Hussein Bashe amesema wameamua kwamba kila Mfanyabiashara anayepewa sukari inayoagizwa kutoka nje majina yapelekwe kwa Wakuu wa Mikoa ili waweze kudhibitiwa kuepusha tabia ya Watu kununua sukari na kuificha ili kuongeza bei.
Akiongea Ikulu Dar es salaam leo, Bashe amesema “Tutaingiza sukari mpaka mwisho wa mwaka huu tutaendelea kuingiza mpaka ambapo tutaona stability ipo, sasa viwanda vinapoleta sukari mpaka kwa Wauzaji wa jumla hatuna changamoto ya kutofuata bei elekezi, shida inaanzia ikienda kwa Wauzaji wa rejareja, na sasa hivi tumeamua kwamba kila anayepewa sukari inayoagizwa kutoka nje tunapeleka majina kwa Wakuu wa Mikoa, kumeibuka tabia ya Watu kuficha sukari Mtu ananunua na anaificha ili kuongeza bei”
“Namshukuru Waziri Mchengerwa kuwaagiza Wakuu wa Mikoa na Wilaya kutumia Kamati zao Ulinzi na Usalama, hii ni hujuma tumewaambia Wamiliki wa viwanda hata wao tutawachukulia hatua wana jukumu la kuwasimamia Wasambazaji wao”
“Soko la sukari sio perfect market ni soko ambalo linalindwa kwahiyo panapotokea crisis Mfanyabiashara yoyote lazima a-take advantage ili bei iende juu, msingi wa bei sokoni kuongezeka ilianzia kiwandani walivyopandisha hadi 2900, Muuza duka wa jumla akaongeza, na wa rejareja akaongeza anavyotaka na nataka niseme kuupasua huu mfumo wao wa usambazaji na biashara yao ya sukari ili Mlaji apate faida ni mapambano na sisi kama Serikali tutakabiliana nayo”
“Ukishamlea sana Mtoto anaamka anapata keki, anapata mboga saba siku ukitaka kumbadilisha inakuwa mtihani kidogo na tumejipanga kufanya hivyo, Msambazaji Kagera Sugar anatoa sukari inaenda Mwanza halafu inarudi Bukoba sio akili, halafu yule Mtu wa Mwanza ndiye Msambazaji Mwanza, Bukoba, Mara, Shinyanga, Tabora, Kigoma, Rukwa, Katavi karibu 33% ya population ya Nchi hii inahudumiwa na Mtu mmoja, tumelifanyia kazi ili kudhibiti hili”