Jeshi la Polisi Mkoa wa Mjini Magharibi linawashikilia watuhumiwa kwa kosa la kufanya kitendo chenye kuleta maudhi kwa jamii.
Baada ya kusambaa video clip kwenye mitandao ya kijamii ikiwaonesha wananchi hao ambao walirekodi video wakiwa wanaonesha sehemu zao za siri huku wamepikiwa kwenye pikipiki yenye namba za usajili Z.455 LN aina ya TVS ikiendeshwa na Mohd Shaib Mohd (35) Mshirazi na mkaazi wa Magomeni Zanzibar
Kwenye tukio hilo waliopakiwa na Sabrina Samweli Thomas (21) Mmakonde na mkaazi wa shakani na Asia Salum Juma (23) Mndengereko na mkaazi wa shakani ambae kwenye video hiyo alionekana kuvua nguo hadharani wakati alipopakiwa.
Tukio lilitokea usiku katika barabara ya Kiembe Samaki Wilaya ya Magharibi B” Mkoa wa Mjini Magharibi Jeshi la Polisi baada ya kupata taarifa hiyo lilifanya tukio hilo ili kuwabaini mnamo tarehe 22/02/2024 majira ya saa 5:00 usiku lilifanikiwa kuwakamata. watuhumiwa hao.
Aidha juhudi za kuwabaini na kuwakamata watuhumiwa wengine walioshiriki katika tukio hilo zinaendelea
Tazama hapa…