Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa Chama cha Mapinduzi na Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM ya Taifa Mohammed Ali Kawaida ameshiriki Mazishi ya aliyekuwa Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Tabora na Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM ya Taifa Ndg Mohamed Hassan Wakasuvi tarehe 24 Februari, 2024 kata ya mabama Wilaya ya uyui – Tabora.
Ikumbukwe, Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa Chama cha Mapinduzi alikuwa na ziara ya Kamati ya utekelezaji UVCCM Taifa Mkoa wa Kilimanjaro, hivyo amesimamisha ziara ya Kamati ya utekelezaji UVCCM Taifa tarehe tarehe 24 Februari 2024 ili kumpa heshima za mwisho aliyekuwa Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Tabora na Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM ya Taifa.