Mkuu wa Wilaya ya Kilombero *Mhe.Danstan Kyobya leo tarehe ametembelea kijiji cha kibaoni na kutatua mgogoro wa ardhi kati ya serikali ya kijiji cha kibaoni na msikiti( Masjid Qubba).
Akiwa katika kikao cha maendeleo cha kata ya kibaon Mhe.Mkuu wa Wilaya alipokea malalamiko kutoka kwa Imamu wa msikiti huo kuhusiana na eneo hilo na upatikanaji wa hati miliki. Ambapo Mhe.DC aliahidi kutembelea siku ya leo tarehe 19.02.2024.
DC Kyobya amefika msikitini hapo akiambatana na Katibu Tarafa ya tarafa ya Ifakara Bi.Irene Shija na timu ya wataalamu wa Idara ya Ardhi Kilombero.
Kwa Upande wa Serikali ya Kijiji walikuwepo Maafisa watendaji kata na kijiji, Mwenyekiti wa Kijiji na wenyeviti wote wa vitongoji vya kijiji cha kibaoni.
Baada ya kupata maelezo ya kina kwa pande zote na Ushauri wa Wataalamu wa Idara ya ardhi. Ameridhia eneo la Msikiti lipimwe na wapatiwe hati miliki
Akiongea na Viongozi wa Serikali ya Kijiji na Waumini wa Dini ya Kiislamu wanaofanya Ibada zao kwenye Msikiti huo amesema Eneo la Msikiti litapimwa ndani ya mwezi mmoja hati miliki ya eneo hilo iwe imepatikana
Pia Mhe. DC amesema Amani ya nchi hii inategemea zaidi viongozi wa Dini katika kuwahubiria waumini wake hivyo Serikali inathamini kazi ya viongozi wa dini.
Aidha amemuelekeza Imamu wa Msikiti huo kuandaa siku maalumu kwa ajili ya Harambee ya Uchangishaji pesa na vifaa vya ujenzi wa msikiti huo huku Mhe.Mkuu wa Wilaya ameahidi kuchangia Mifuko ya Sementi Hamsini(50) ikiwa ni mchango wake wa awali, Pia amewataka wadau n a wahisani mbalimbali kumuunga mkono katika kuchangia ujenzi wa msikiti huo.
Kwa Upande wake Imamu wa Msikiti Qubba Sheikh Kanduru kwa niaba ya waumini wa Msikiti huo amemshukuru Mhe.Mkuu wa Wilaya kwa ufanyaji kazi wake uliotukuka na kujitoa kwa wananchi wake wote pasi na kubagua Dini ,kabila ,Umri N.k