Waziri Mkuu Kassim Majaliwa ameanza ziara ya siku tano mkoani Mara wenye lengo wakusikiliza changamoto mbalimbali mkoani hapo.
Majaliwa ameanza ziara hiyo leo Februari 26 hadi 30 akitembelea miradi na ufunguzi wa miradi mbalimbali ikiwemo shule za msingi na sekondari
Katika ziara hiyo iliyoanzia wilaya ya Bunda amesikiliza changamoto mbalimbali ikiwemo ya mama mmoja aliyefahamika kwa jina moja la Flora amesema mumewe alitekwa tangu mwaka jana Desemba 10, 2024 na gari namba T647DVF.
Baada ya kusikiliza changamoto hiyo Waziri Mkuu alitoa agizo kwa Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mara, Salum Morcase kuongeza jitihada za kufatilia tukio hilo la mwanaume aliyetekwa.
Baada ya Waziiri Mkuu kutoa maagizo hayo Kamanda wa Polisi Mkoa huo amesema Salum Morcase amesema suala hilo wanalifahamu na wanalifuatilia.