Uchunguzi umefunguliwa kuhusu majibu ya fowadi wa Al-Nassr, Cristiano Ronaldo, kwa kejeli za ‘Messi’.
Ronaldo alifunga bao wakati timu hiyo ya Saudi Arabia ilipoilaza Al-Shabab 3-2 katika mchezo wa ligi Jumapili.
Baada ya mchezo huo, video iliyoibuka kwenye mitandao ya kijamii ilimuonyesha nahodha huyo wa Ureno akiwaelekeza baadhi ya watu kwenye umati baada ya kufunga penalti.
Huku wafuasi wengi vijana wakihudhuria, viongozi katika Mashariki ya Kati wamehimizwa kuchukua hatua.
Al-Nassr wanataka kumtetea Ronaldo dhidi ya kosa lolote, lakini Kamati ya Nidhamu na Maadili ya Shirikisho la Soka la Saudi imefungua kesi na itachunguza ushahidi wote uliopo kabla ya kufanya uamuzi wa nini kitafuata.