Paul Edmonds, mwanamume kutoka jimbo la California la Marekani ametambuliwa kupona saratani na VVU baada ya matibabu mahususi miaka mitano iliyopita yanayojulikana kama upandikizaji wa seli .
Mnamo 2021, pia alikua mmoja wa watu watano ulimwenguni ambao walikuwa wameponywa VVU.
Akishiriki hadithi yake na Taasisi ya Kitaifa ya Saratani, Edmonds alisema kwamba alikuwa akiishi na VVU-1 kwa miaka 31 kabla ya upandikizaji.
“Watu walikuwa wakifa ndani ya miaka michache baada ya kujua kwamba walikuwa na virusi,” alisema Edmonds akikumbuka kusoma kumbukumbu za marafiki wengi huko nyuma katika miaka ya mapema ya 1980.
Edmonds aligunduliwa mnamo 1988 na sio tu VVU, lakini UKIMWI kamili. Aliliambia Jiji la Matumaini, kwamba alihisi amepewa hukumu ya kifo.
Mnamo 1997, alianza tiba ya kurefusha maisha ya VVU , lakini kwake aliona sio tiba.
Kuhusu matibabu
Edmonds amepatikana hana saratani wala VVU baada ya matibabu hayo mahususi na sasa anasema anaona ni kama msamaha aliopata wa kuanza maisha mapya .
Yeye sio tu mtu wa tano ulimwenguni kupona VVU, lakini pia ni mzee na alikuwa na VVU kwa muda mrefu zaidi.
Edmonds, 67, na mkewe Arnie House, wote walikuwa na VVU walipogunduliwa kwa mara ya kwanza zaidi ya miongo mitatu iliyopita.
“Sikuwa tayari kufa,” aliiambia ABC News, akizungumza kuhusu matibabu yake ya kimiujiza katika City of Hope.
Timu ya matibabu nyuma ya kesi yake ilichapisha kupona kwake kwa kushangaza katika Jarida la New England la Tiba.