Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) leo kinahitimisha maandamano yake jijini Arusha ikiwa ni takribani siku 33 tangu kilipoanza kuandamana katika majiji Januari 24, mwaka huu.
Maandamano hayo yanayoongozwa na viongozi wa kitaifa, akiwamo Mwenyekiti wa chama hicho, Freeman Mbowe, yanalenga kushinikiza serikali kuondoa bungeni miswada mitatu ukiwamo wa mabadiliko ya sheria za uchaguzi, kuboresha katiba mpya na mambo mengine.
Katibu wa chama hicho Kanda ya Kaskazini, Amani Golugwa, amesema jijini Arusha kuwa maandalizi yote ya maandamano jijini humo yamekamilika. “Sisi kama chama, tunahuzunika na waliopata msiba huu mzito na tumetoa pole kwa wafiwa.