Ni February 27, 2024 ambapo Wajumbe wa Kamati ya Utekelezaji ya Baraza kuu la UVCCM Taifa wakiongozwa na Mwenyekiti UVCCM Taifa Ndugu Mohammed Ali Kawaida (MCC) Mradi wa ujenzi wa Shule ya Sekondari iliyopo Mkundi inayotarajiwa kugharimu zaidi ya Tsh. 500 Milioni mpaka kukamilika kwake, mpaka sasa tayari washatumia 300 Milioni na ujenzi unaendelea.
Kamati ya utekelezaji imeridhishwa na ujenzi wa wa shule hiyo kwani wananchi wa mkundi walikuwa wanateseka watoto wao walikuwa anatembea 18 Km kwenda shuleni na 18Km kurudi nyumbani jumla 36Km.
Mwenyekiti amewasisitiza wasimamizi wa mradi kuharakisha ujenzi ili wananchi kutatuliwa kero hiyo kama ilivyo dhamira ya Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kusogeza huduma karibu na Wananchi.