Ni February 27, 2024 ambapo Wajumbe wa Kamati ya Utekelezaji ya Baraza kuu la UVCCM wakiongozwa na Mwenyekiti UVCCM Taifa Ndugu Mohammed Ali Kawaida (MCC) yakabidhi kadi 516 kwa wanachama wapya pamoja na mashina ya kuchakata kokoto na mizinga 40. Mashine ya kuchakata kokoto inagharimu zaidi ya Tsh. Milioni sita 6,000,000/= imekabidhiwa kwa vijana wa kata ya Mnazi na Mizinga 40 ya kufuga nyuki inagharimu Tsh. 3,200,000/=, mizinga 20 zilikabidhiwa kwa vijana wa kata ya Mbaramo na 20 kata ya Sahagayu wilayani Lushoto.
Kamati ya utekelezaji kupitia Mwenyekiti wake baada ya kukabidhi vifaa hivyo kwa vijana wa CCM aliwasihi kutumia vifaa hivyo kujikwamua kiuchumi na ikawe sehemu ya kuwaunganisha vijana wote katika umoja wao, isije kuwa sehemu ya vijana kulumbana na kuchukiana.