Serikali ya Tanzania imeshauriwa kuwaongezea utashi walimu na wanafunzi wa shule zote za Serikali na Binafsi katika kuandaa kesho iliyobora zaidi kwani utaweza kuwaongezea uwezo mkubwa wa kufikiri.
Kauli hiyo imesemwa na miongoni mwa wazazi wa mwanafunzi kutoka katika shule ya GENESIS wakati wa maonesho sayansi na teknolojia ya Wanafunzi kwa mwaka 2024 iliyofanyika Jijini Dar es salaam.
” Hii ni nzuri kufanya hata Shule za Serikali kwani inawaongezea maarifa zaidi Walimu na Wanafunzi na haina Gharama kubwa sana, hii pia inasaidia kuishi bila kutegemea Ajira” Amesema Mzazi wa Mwanafunzi.
Naye mwakilishi wa shule ya GENESIS Ndg. Hassani Massawe akasema kuwa ” Sisi hii desturi yetu na imekuwa ikisaidia sana hawa Wanafunzi katika kuwaongezea maarifa na ubunifu hasa kwa wakati huu wakiwa bado wadogo.
Hata hivyo Mwanafunzi wa Shule hiyo Hamduni Nassoro, ameishukuru Shule yao kwa maonesho hayo ya Sayansi na Teknolojia yanayofanyika kila mwaka kwani kwao imekuwa ni faida kubwa, Lakini ni Fursa kwa Wanafunzi kubadili mawazo ya ubunifu kila mwaka.