Afrika Kusini ilirekodi vifaru 499 waliouawa mwaka 2023, 51 zaidi ya mwaka uliopita, licha ya juhudi za kuwalinda wanyama hao, serikali ilisema Jumanne.
Afrika Kusini ni nyumbani kwa karibu nusu ya vifaru weusi walio katika hatari kubwa ya kutoweka barani Afrika na kwa idadi kubwa zaidi ya vifaru weupe wanaokaribia hatarini.
Vifaru huwindwa kwa ajili ya pembe zao, ambazo hutumiwa katika nchi za Asia mashariki kutengeneza dawa za kienyeji na vito.
Mwaka 2023, vifaru 406 waliuawa kwenye mali ya serikali na 93 kwenye mbuga, hifadhi na mashamba ya watu binafsi, Idara ya Misitu, Uvuvi na Mazingira ya Afrika Kusini ilisema katika taarifa yake.