Liverpool na Manchester City wanafikiria kumsajili kiungo wa FC Porto Alan Varela, linasema jarida la Ureno O Jogo.
Varela, 22, ameshinda sifa kwa mtindo wake wa ukali katika safu ya kati na alicheza jukumu kubwa katika kuishinda Arsenal katika mechi ya mkondo wa kwanza ya hatua ya 16 ya Ligi ya Mabingwa wiki iliyopita.
Mchezaji huyo wa kimataifa wa Argentina U20, ambaye amefananishwa kwa mtindo na Javier Mascherano, alisajiliwa na Porto kwa takriban €11m kutoka Boca Juniors majira ya joto yaliyopita, lakini tayari amekuwa akihusishwa na kuhamia Ligi ya Premia na inasemekana ana kipengele cha kutoa €70m. mkataba wake.