Mama mmoja ashtakiwa kwa mauaji ya mtoto wake wa kiume mwenye umri wa miaka mitatu baada ya kutumia kumpiga kwa fimbo kupitiliza nakudai kuwa ni kwa sababu Biblia ilimwambia ni sahihi “kumwadhibu mtoto wake”, mahakama imesikiliza.
Christina Robinson, 30, aliita huduma za dharura nyumbani kwake katika Mahakama ya Bracken, Durham, mnamo Novemba 2022 na kudai Dwelaniyah alikuwa amelegea na kudondoka.
Richard Wright KC, mwendesha mashtaka, aliiambia Mahakama ya Crown ya Newcastle mvulana huyo alipata jeraha baya kichwani baada ya kutikiswa kwa nguvu na mama yake.
Upande wa mashtaka ulisema miguu ya mtoto huyo ilikuwa imefungwa bandeji nyingi, kuficha majeraha ya moto ambayo yalifunika hadi asilimia 20 ya mwili wake na yalimsababishia maumivu makali kwa wiki kadhaa kabla ya kifo chake, baada ya kuchomwa kwa nguvu na makusudi na mama yake bafuni.
Mwendesha mashtaka alisema: “Mshtakiwa sasa anadai kwamba kumpiga mtoto kwa fimbo ili atoe damu kulitokana na yeye kuwa mfuasi wa mafundisho ya Biblia.”
Robinson amekanusha kumuua Dwelaniyah na kufanya ukatili kwa watoto.