Wakazi wa vitongoji viwili katika eneo la Bambo, huko Bwito katika jimbo la Rutshuru (Kivu Kaskazini) wamelazimishwa kuhama makaazi yao kwa maagizo ya waasi wa M23. Kulingana na Radio OKAPI ikinukuu viongozi wa kimila katika eneo hilo, kaya mia tano katika wilaya za Lubango na Makengele ndio wamehamishwa.
Wakazi hawa walihamishiwa katika eneo la Bugina, katika jimbo jirani la Tongo, na wengine kusini mwa eneo la Bambo.
Kulingana na watu viongozi wa eneo hilo, vitongoji viwili vinapakana na nafasi ya kimkakati ya waasi, ambao wanakabiliana na FARDC katika eneo hili.
Hadi siku ya Jumatano, ufikiaji wote katika vitongoji hivi viwili ulikuwa bado ni marufuku kabisa, vinasema vyanzo hivyo, ambavyo vinapingana na uhamishaji huu wa kulazimishwa wa wakaazi.
Wakaazi hawa sasa wanashi bila usaidizi na bila njia zingine za kuishi.
Kuhamishwa kwa watu hawa kumesababishwa na shambulio la kuvizia, lililotekelezwa na wanaodhaniwa kuwa wapiganaji wa ndani, dhidi ya doria ya waasi kutoka eneo hili, wakati wa usiku wa Jumamosi kuamkia Jumapili wiki iliyopita.