Rais wa Club ya Yanga Injinia Hersi Said leo akihojiwa na AlAhly TV Nchini Egypt, amesema Rais Samia Suluhu Hassan yupo nyuma ya mafanikio ambayo yanashuhudiwa kwenye mpira wa miguu Nchini Tanzania kwa sasa kutokana na jitihada zake kwenye kuliunga mkono soka.
“Kama ukinuliza mimi kuhusu mafanikio ya soka la Tanzania nitasema ni Rais wa Nchi, yeye ndio yuko nyuma ya kila kitu kinachotokea hata kufuzu kwa Timu ya Taifa ya Tanzania kwenye mashindano ya AFCON 2023 ni kwa sababu ya Rais wetu, yuko nyuma ya kila kitu” – Hersi.
Injinia Hersi alisema kwamba hata kitendo cha Uganda, Kenya na Tanzania kuandaa mashindano ya AFCON 2027 ni mpango wa Rais Samia Suluhu Hassan—“Yeye ndio yupo nyuma ya kila mafanikio yanayotokea Nchini Tanzania, Yanga kwenda kwenye fainali ya CAF Confederation ni kwa sababu yake, alikua akitu-support kwenye kila hatua na hata kulipa bonus kwa Wachezaji kwa kila goli watakalofunga na hata tulipokwenda kwenye fainali Algeria alitupa Ndege yake ( kutoka AirTanzania) na ikatusubiri wakati wote kwahiyo ukinuliza Mtu ambaye yupo nyuma ya mafanikio ya soka Tanzania ni Rais wetu Madame Samia Suluhu Hassan” ——— Rais wa Yanga, Hersi Saidi.