Rais wa Club ya Yanga Injinia Hersi Said leo akihojiwa na AlAhly TV Nchini Egypt, amesema Rais Samia Suluhu Hassan yupo nyuma ya mafanikio ambayo yanashuhudiwa kwenye mpira wa miguu Nchini Tanzania kwa sasa kutokana na jitihada zake kwenye kuliunga mkono soka.
“Chachu ya mafanikio ya mpira wetu Tanzania ni Rais wetu Mhe. Samia Suluhu Hassan, Rais wetu amekuwa na mchango mkubwa sana kwenye soka la nchi yetu“-
“Taifa Stars kufuzu kwenda kwenye fainali za AFCON 2023 nchini Ivory Coast ni moja katika mafanikio yake, Kufaulu kwa UMOJA BID katika kuandaa AFCON 2027 ni sehemu kubwa ya jitihada za Rais Samia Suluhu Hassan”-
“Aidha mchango wake mkubwa katika kujenga Hamasa kupitia “GOLI LA MAMA” umeifikisha Young Africans katika fainali ya kombe la Shirikisho barani Afrika 2022/23 na sasa Young Africans kufuzu kwenda robo fainali ya Klabu bingwa barani Afrika”-
“Aidha mchango wake mkubwa katika kujenga Hamasa kupitia “GOLI LA MAMA” umeifikisha Young Africans katika fainali ya kombe la Shirikisho barani Afrika 2022/23 na sasa Young Africans kufuzu kwenda robo fainali ya Klabu bingwa barani Afrika,Asante Sana Mama” Amesema Rais wa Young Africans Eng.Hersi Ally Said kwenye Kituo cha Televisheni cha @alahlytv Cairo, Egypt