Serikali ya Marekani, kupitia Taasisi ya Kijeshi ya Utafiti wa Maradhi ya Walter Reed (Walter Reed Army Institute of Research, WRAIR-DoD) imekabidhi kwa Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) majengo mawili ya maabara yaliyokarabatiwa katika Zahanati ya Makambako mkoani Njombe na Hospitali ya Kijeshi ya Mbalizi mkoani Mbeya.
Hafla ya makabidhiano ilifanyika katika Hospitali ya Kijeshi ya Mbalizi ikihudhuriwa na Brigedia Jenerali wa JWTZ Charles Mwanziva, Mwambata wa Kijeshi wa Ubalozi wa MarekaniLuteni Kanali Gerald Mathis, Mkurugenzi Mkazi wa WRAIR-DoD Tanzania, Mark Breda na Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Kimataifa ya Utafiti wa Kimatibabu ya Henry M. Jackson Foundation Medical Research International (HJFMRI), Sally Talike Chalamila.
Serikali ya Marekani kupitia Mpango wa Dharura wa Rais wa Marekani wa Kukabiliana na UKIMWI (PEPFAR) ni mfadhili mkubwa zaidi wa jitihada za kupambana na VVU/UKIMWI nchini Tanzania.
Leo hii, PEPFAR nchini inawasaidia zaidi ya watu milioni 1.5 kupata matibabu ya kufubaza VVU yanayookoa maisha.
Taasisi ya WRAIR-DoD imekuwa ikiendesha shughuli zake nchini Tanzania toka mwaka 1999, ikijielekeza katika jitihada za kutokomeza VVU kupitia utafiti na utekelezaji wa programu mbalimbali za PEPFAR za kinga, matunzo na matibabu kwa rai ana askari.
Toka mwaka 2006, Marekani imetoa matibabu kwa jumla ya wagonjwa 23,730 ambao asilimia 88 miongoni mwao wameweza kufikia hatua ya virusi kufubazwa kabisa na hivyo hawawezi kuwaambukiza wengine.
Akizungumza katika hafla hiyo, Brigedia Jenerali Charles Mwanziva alisema “NaishukuruWRAIR-DoD kutoka Ubalozi wa Marekani, wanaofadhili mradi wa HJFMRI, ambao unatekeleza kwa mafanikio afua mbalimbali za VVU katika vituo vyetu vya afya vya kijeshi vipatavyo 21.
Naye Mwambata wa Kijeshi wa Ubalozi wa Marekani, Luteni Kanali Gerald Mathis alisema, “Kupitia ufadhili wa Mfuko wanDharura wa Rais wa Marekani wa Kupambana na UKIMWI (PEPFAR), WRAIR-DoD itaendelea kulisaidia Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanznia (JWTZ) katika kutoa huduma bora za kupambana na VVU/UKIMWI katika hospitali na vituo vyote vya
afya vya kijeshi 21 nchini Tanzania ili kufikia malengo Shirika la Umoja wa Mataifa la Kupambana na UKIMWI”