Wakati kesi ya mauaji dhidi ya Mwanariadha Oscar Pistorius ikiendelea leo nchini Afrika Kusini, ripoti ya kiuchunguzi juu ya afya yake ya akili imetolewa ambapo imebainisha kuwa mwanariadha huyo hakuwa na ugonjwa wa akili wakati akimuua mpenzi wake.
Upande wa mashtaka umesema kuwa kutokana na ripoti hiyo inamaanisha mwanariadha huyo alifanya uhalifu huo kwa makusudi wakati akimpiga risasi mpenzi wake.
Upande wa utetezi ulidai kuwa Pistorius alipatwa na ugonjwa kwenye akili yake wakati akitekeleza tukio hilo.
Mwanariadha huyo anakana vikali kumuua mpenzi wake Reeva Steenkamp ambapo anasema alimpiga risasi kwa bahati mbaya akidhania ni mvamizi ameingia ndani ya nyumba yake.
Upande wa mashtaka unadai kuwa Pistorius alimuua kwa makusudi Steenkamp baada ya majibizano.
Pande zote mbili yaani upande wa mashtaka na upande wa utetezi umeikubali ripoti hiyo iliyowasilishwa mahakamani.
Ni halali yako kupata kila stori inayonifikia mtu wangu, niko tayari kukutumia wakati wowote kupitia twitter instagram na facebook ukijiunga na mimi kwa kubonyeza >>> twitter Insta FB