Ripoti kutoka N’Djamena zinaarifu kuwa kiongozi wa Upinzani nchini humo ,Yaya Dillo ameuawa katika mapigano na vikosi vya usalama.
Taarifa zinasema kuwa Dillo aliuawa kwa kupigwa risasi na askari usalama jana Alhamisi.
Yaya Dillo alikuwa akituhumiwa na serikali ya Chad kwa kushiriki katika shambulio kubwa dhidi ya wakala wa usalama wa ndani katika mji mkuu wa nchi hiyo; tuhuma ambazo alizikanusha. Mashambulizi makali ya ufyatuaji risasi yalijiri jana karibu makao makuu ya chama alichokuwa akiiongoza kiongozi huyo wa upinzani huko N’Djamena.
Dillo ambaye alikuwa mkosoaji mkubwa wa Rais Mahamat Deby wa Chad alimpinga Rais huyo wa serikali ya mpito ya Chad tangu ashike hatamu za uongozi mwaka 2021akimrithi baba yake, Idriss Deby ambaye aliuawa na waasi baada ya kutawala kwa miaka thelathini.