Waziri wa Mipango na Uwekezaji Profesa Kitila Mkumbo amesema kuwa Serikali imeweka mazingira mazuri ya biashara hivyo sekta ya bima ni moja ya fursa katika kutoa huduma kwa wananchi katika ukuaji wa uchumi.
Kitila ameyasema hayo wakati wa kusherehekea miaka 25 kampuni ya Bima ya Icea Lion iliyofanyika Hyatt Regency Hotel jijini Dar es Salaam.
Amesema miaka 25 ya kusherekea hatua ya kwenda kusherekea miaka 50 hadi 100 kutokana na serikali kuweka mazingira wezeshi ya kufanya biashara nchini.
Amesema kuwa kuna miradi mikubwa ya serikali ya mikakati ambapo bima ni fursa kwao kutokana huduma zinazotolewa na kampuni mbalimbali.
Profesa Kitila amesema kuwa Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan amefungua milango ya biashara ambayo inaongeza ajira kwa wananchi.
Kwa upande wa Mkuu wa Wilaya ya Ilala Edward Mpogolo amesema wakati umefika kwa Icea Lion kushirikiana kutoa elimu kuhusiana na bima za ajali za moto na wilaya iko tayari kutoa ushirikiano huo.
Amesema kuwa mkoa wa Dar es Salaam na jiji la Biashara ambapo sekta ya bima ina umhimu sana.
Mkurugenzi Mtendaji wa Icea Lion Jared Awando amesema miaka 25 hadi kusherekea miaka hiyo ni milima mabonde lakini wateja wameendelea kutoa ushirikiano wa huduma za Icea Lion.
Awando amesema kuwa katika kusherekea huko wanaanza hatua nyingine miaka mingine ambayo itakuwa na matokeo mazuri zaidi kutokana na mikakati iliyowekwa katika kutoa huduma za bima nchini.