Maelfu ya wafungwa walitoroka katika gereza moja nchini Haiti baada ya magenge yenye silaha kuvamia kituo hicho siku ya Jumapili.
Wafuasi wa genge hilo walivamia Gereza la Croix des Bouquets katika mji mkuu wa Port-au-Prince, na kusababisha makabiliano na vikosi vya usalama.
Wakati wa vita, wafungwa 3,600 walitoroka, huku 12 wakiuawa.
Serikali ya Haiti ilitoa taarifa ikisema kwamba mashirika ya uhalifu yalishambulia gereza hilo asubuhi na mapema, na kwa sababu ya upinzani wa polisi, watu wenye silaha walikimbia eneo hilo.
Waziri Mkuu wa Haiti Ariel Henry yuko nje ya nchi kwa sasa.
Alienda wiki iliyopita nchini Kenya, ambapo alisaini makubaliano ya pande mbili kuruhusu maafisa 1,000 wa polisi wa Kenya ambao wataongoza kikosi cha usalama cha kimataifa.
Umoja wa Mataifa uliidhinisha kikosi hicho kusaidia Haiti kupambana na vurugu za makundi yenye silaha na kurejesha usalama. Haikuwa wazi alikokuwa waziri huyo mkuu Jumapili.
Wafungwa 99 walibakia ndani ya gereza ambapo awali lilikuwa na karibu wafungwa 4,000.