Haiti imetangaza hali ya tahadhari ya saa 72 na amri ya kutotoka nje usiku ndani na karibu na mji mkuu kwa sababu ya kuvamiwa kwa magereza mawili na ukosefu wa usalama unaoendelea.
Mwishoni mwa juma, magenge yenye silaha yalivamia gereza kubwa la Port-au-Prince, na kusababisha mauaji ya takriban watu 12 na kuachiliwa kwa karibu wafungwa 4,000.
Viongozi wa magenge wanasema wanataka kumlazimisha Waziri Mkuu Ariel Henry, ambaye yuko nje ya nchi ajiuzulu.
Idadi kubwa ya wanaume wapatao 4,000 waliokuwa wameshikiliwa humo sasa wametoroka, mwandishi wa habari wa eneo hilo kulingana na BBC.
Miongoni mwa waliozuiliwa ni wanachama wa genge walioshtakiwa kuhusiana na mauaji ya mwaka 2021 ya Rais Jovenel Moïse.
Ghasia nchini Haiti, ambayo ni nchi maskini zaidi katika bara la Amerika, zimezidi kuwa mbaya katika miaka ya hivi karibuni. Magenge yanayolenga kumtimua Waziri Mkuu Ariel Henry yanadhibiti 80% jiji la Port-au-Prince.