Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara Exaud Kigahe Akimwakilisha Naibu waziri Mkuu na Waziri wa Nishati amemuagiza Mkuu wa Mkoa wa Geita Martine Shigela kwa kushirikiana na wakuu wa wilaya zote kuhakikisha wanazunguka Mkoa wa Geita kwa ajili ya kutatua changamoto zinazowakabili wafanyabiashara wa katoro pamoja na wananchi wa Maeneo mbalimbali.
Akizungumza Mara Baada ya kusikiliza kero za Wafanyabiashara hao katika kikao kilichokuwa kimeandaliwa kwa lengo la kutatua changamoto zinazowakabili wafanyabiashara hao Naibu waziri Kigahe ameigiza Pia Maafisa Biashara katika halmashauri zote nchini kuhakikisha wanasimamia vyema na kutoa huduma nzuri kwa wafanyabiashara ikiwemo suala la elimu ya Mikopo ya asilimia 10.
” Lakini pia nitumie nafasi hii sababu Mkuu wa wilaya yetu yuko hapa ambaye anamwakilisha Mkuu wa mkoa na Amesema kwamba kuanzia kesho kadri ratiba zilivyopanga wataanza kutembelea katika Mkoa huu na wataanzia hapa katoro naomba sana mkazishughulikie kwa haraka na kwa umakini sana changamoto ambazo wafanyabiashara hawa wakatoro wamezisema, ” Naibu Waziri Kigahe.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya ya Geita , Charles Kazungu ameseikitishwa na maagizo yaliyowahi kutolewa katika kikao cha Balaza la Madiwani kupitia Kamati ya Fedha kushindwa kutekelezwa likiwemo suala la Wafanyabiashara kupangishwa katika vibanda vinavyomirikiwa na Serikali.
Naye Mbunge wa Jimbo la Busanda Tumain Magesa na Mbunge wa Jimbo la Geita Joseph Kasheku wamempongeza Naibu waziri kwa kufika katika kusikiliza kilio cha wafanyabiashara hao huku wakimuomba kukaa na Maafisa Biashara kutoa elimu kwa wafanyabiashara hao pale wanapopata nafasi ya kuwatembelea.
Charles Makanji ni Mwenyekiti wa Wafanyabiashara Katoro ametuhumu kuwepo kwa Baadhi ya Maafisa Biashara ambao wamekuwa mstari wa mbele kuweka Masilayi yao Binafsi na kutokweka Masilayi ya Serikali mbele ikiwemo tuhuma ya uwepo wa Vibanda vilivyokuwa vikimilikiwa na Serikali kumilikiwa na Mwananchi.