Mamia ya watu wamekusanyika katika mji mkuu wa Senegal Dakar kutaka uchaguzi wa rais wa nchi hiyo ufanyike kabla ya Aprili 2, tarehe ambayo ndipo unapomalizika muhula wa rais wa hivi sasa, Macky Sall
Nchi hiyo ya magharibi mwa Afrika Magharibi ilitumbukia kwenye mgogoro wa kisiasa tarehe 3 mwezi uliopita wa Februari wakati Macky Sall alipoakhirisha uchaguzi wa rais uliokuwa umepangwa kufanyika Februari 25.
Hatua hiyo ililaaniwa na wapinzani kuitwa ni mapinduzi ya katiba, na ilizusha maandamano makubwa ambayo yamesababisha vifo vya watu wanne.
Hatimaye Baraza la Katiba lilitengua hatua hiyo ya Rais Sall na tangu wakati huo Senegal imekuwa ikingojea tarehe mpya ya uchaguzi.