Mwanaume mmoja wa India alikamatwa kwa kuvaa sare ya polisi na kujifanya afisa wa polisi ili kumsaidia dadake kufanya udanganyifu katika mtihani wake wa shule ya sekondari.
Mitihani ya Cheti cha Juu cha Sekondari (HSC), wakati muhimu kwa wanafunzi katika jimbo lote la Maharashtra nchini India na ilianza Februari 21,.
Mwanamume huyo mwenye umri wa miaka 24 aliingia katika Shule ya sekondari ya Shahbabu Urdu katika mji wa Patur akiwa amevalia sare ya polisi ya khaki akiwa na lengo la wazi kabisa – kumsaidia mwanafunzi mmoja kufaulu mtihani huo mgumu kwa kupita karatasi zake za udanganyifu.
Alipanga kujipenyeza kwenye kituo cha mitihani kwa kisingizio cha kuwasimamia wanafunzi na kumpa dada yake taarifa zinazohitajika ili kufaulu mtihani huo ni mambo pekee ambayo hayakuwa sawa kama ilivyopangwa walisema polisi.