Baada ya kuwepo taarifa katika mitandao ya kijamii kuwa Bandari ya DSM shughuli zimesimama kwa siku ya pill na Gati zote hazifanyi kazi na hiyo imetokana na Mwekezaji DP World kuvunja mikataba kwa Wafanyakazi.
AyoTV imefika Bandari ya DSM na kuzungumza na Mkurugenzi wa Bandari hii Mrisho Mrisho ambapo amesema Taarifa hizo ni za uzushi na DP World bado hawajaanza shughuli katika Bandari ya DSM.
“DP World bado hawajaanza kazi lakini wataanza hivi karibuni, Watanzania wapuuze hizo taarifa ni za uzushi, taarifa zenye kuleta taharuki kwa watumiaji wa Bandari, Bandari haijawahi kusimamisha shughuli zake hata kidogo, ukiona imesimama watu wanabadili shift, tuna shift tatu asubuhi, mpaka jioni, jioni mpaka Usiku wengine wanamalizia asubuhi tunafanya kazi Saa 24” Mrisho
“Bandari hakuna mgomo wafanyakazi wanaendelea na majukumu yao, ni dharau ukisema wamegoma wana hari kubwa sana hawajawahi kugoma wala kufikiria kugoma” Mrisho
Suala la Wafanyakazi kuvunjiwa mikataba Mrisho amesema “hilo halipo nalo halina ukweli kwasababu mikataba ni mambo ya ndani, DP World kuleta wafanyakazi wapya hilo nalo halipo”
Kuhusu upendeleo kutoa mizigo Mrisho amesema hakuna upendeleo meli inayowahi kufika ndio inahudumiwa ila kuna nyakati za udharura mfano wakati wa sukari.
“Upangaji wa meli unahusisha wale wenye meli kila siku wanakutana, hilo nalo uongo kuna nyakati za dharura mfano Nchi inajua kuna tatizo la sukari, meli ya sukari ikiingia tunaipa kipaumbele, Mwenye meli tunawaambia” Mrisho