Ujumbe wa msaada kwa hospitali mbili kaskazini mwa Gaza ulipata matukio ya kutisha ya watoto wakifa kwa njaa, huku kukiwa na uhaba mkubwa wa chakula, mafuta na madawa, Shirika la Afya Duniani limesema.
Matokeo hayo yalikuwa “ya kusikitisha”, mkuu wa WHO Tedros Adhanom Ghebreyesus alisema kwenye X, akiongeza kuwa “hali ya Al Awda ilikuwa ya kutisha sana, kwani moja ya majengo yameharibiwa”.
Hospitali ya Kamal Adwan, hospitali pekee ya watoto kaskazini mwa Gaza, ilizidiwa na wagonjwa, alisema. “Ukosefu wa chakula ulisababisha vifo vya watoto 10,” Tedros alisema.