Mamlaka ya Nigeria imekamata malori 21 yakiwa yamepakia vyakula na bidhaa zisizo za vyakula zikielekea nchi jirani za Chad na Cameroon pamoja na Jamhuri ya Afrika ya Kati.
Haya yanajiri wakati Nigeria inakabiliwa na mzozo wa kiuchumi ambao haujawahi kushuhudiwa na kupanda kwa bei ya vyakula na kushuka kwa thamani ya sarafu.
Malori hayo yalikamatwa ”katika operesheni kali” kando ya mpaka wa jimbo la Borno kaskazini mashariki mwa Nigeria siku ya Jumanne, shirika la kupambana na ufisadi nchini humo, Tume ya Uhalifu wa Kiuchumi na Kifedha, EFCC, ilisema katika taarifa.
Haijafichua haswa aina za vyakula na vitu visivyo vya chakula ambavyo vilizuiliwa.
Idadi isiyojulikana ya washukiwa wamekamatwa na watashtakiwa mahakamani baada ya uchunguzi, EFCC iliongeza. Haijabainika mara moja kile kinachomkera mshukiwa huyo kwa vile mauzo ya chakula kutoka Nigeria kwa ujumla si haramu.