Juhudi za kupeleka chakula kilichohitajika sana kaskazini mwa Gaza zilianza tena Jumanne lakini “hazikufaulu,” lilisema Shirika la Mpango wa Chakula Duniani (WFP).
Msafara wa lori 14 wa chakula, wa kwanza kwa wakala tangu iliposimamisha usafirishaji kuelekea kaskazini mnamo Februari 20, ulirudishwa nyuma na vikosi vya Israel baada ya kusubiri kwa saa tatu katika kituo cha ukaguzi cha Wadi Gaza, WFP ilisema katika taarifa.
“Ingawa msafara wa leo haukufika kaskazini kutoa chakula kwa watu wanaokabiliwa na njaa, WFP inaendelea kutafuta kila njia iwezekanayo kufanya hivyo,” alisema Carl Skau, naibu mkurugenzi mtendaji wa WFP.
Ikisema kwamba njia za barabarani ndio njia pekee ya kusafirisha kiasi kikubwa cha chakula kinachohitajika kuepusha njaa kaskazini mwa Gaza, ilibainisha kuwa mapema siku hiyo, kwa msaada wa Jeshi la anga la Kifalme la Jordan, tani sita za chakula cha WFP kwa watu 20,000 ziliangushwa kaskazini mwa Gaza.
“njia ya anga ni ya mwisho na hayataepusha njaa. Tunahitaji maeneo ya kuingia kaskazini mwa Gaza ambayo yatatuwezesha kufikisha chakula cha kutosha kwa watu nusu milioni wanaohitaji sana,” alisema Skau.