Ripoti zinadai mamlaka ya Uhispania imeomba kifungo cha miaka minne na miezi tisa jela kwa kocha wa Real Madrid Carlo Ancelotti kutokana na ulaghai wa kodi.
Vyombo vya habari vya Uhispania, vikiwemo Relevo na OK Diario, vinaripoti Mwendesha Mashtaka wa Madrid ameomba kifungo cha miaka minne na miezi tisa jela kwa kocha wa Real Madrid Carlo Ancelotti.
Kama ilivyoelezwa na Football Espana “mashtaka hayo yanahusiana na ukwepaji kodi, ambapo katika kipindi cha 2013 na 2014, Ancelotti alidaiwa kuweka safu tata na ya kutatanisha ya jumuia za ujenzi ili kuepusha kutozwa ushuru sahihi kwa haki za picha yake katika kipindi hicho.
Inasemekana kwamba Muitaliano huyo ‘aliiga’ utoaji wa haki zake za taswira kwa makampuni mengine ili kuficha mapato.”
Ancelotti, kocha wa zamani wa Milan na Juventus, alijiunga na Real Madrid kwa mara ya kwanza mwaka 2013 na kukaa miaka miwili Bernabeu, na kushinda taji la kihistoria la ‘La Decima’ la 10 la Ligi ya Mabingwa katika historia ya klabu hiyo mnamo 2013-14.
Alirejea katika mji mkuu wa Uhispania mwaka 2021 na hivi karibuni amesaini mkataba wa nyongeza na wababe hao wa La Liga hadi Juni 2026.