Kituo cha Huduma za kisheria (LSF) na Shirika la maendeleo la Ubelgiji, Enabel wamesaini rasmi mkataba wa ruzuku wa bilioni 10.7 za Kitanzania leo kutekeleza Maboresho ya Upatikanaji wa Haki kwa Wanawake kupitia Msaada wa Kisheria.
Akizungumza Mkurugenzi Mtendaji wa LSF, Lulu Ng’wanakilala amesema “Kupitia mradi huu, LSF itahakikisha kuwa huduma za msaada wa kisheria zenye ubora zinapatikana kwa watu wote kupitia mifumo rasmi na isiyo rasmi ya utoaji haki. Lulu amefafanua zaidi kuwa mradi huu utaongeza uelewa wa jamii hususani wanawake na wasichana kuhusina na umhimu wa msaada wa kisheria katika.”
Naye Mwakilishi Mkazi wa Enabel nchini Tanzania, Koenraad Goekint, amesisitiza kusema “Tunafurahi kuanzisha ushirikiano huu muhimu na Kituo cha Huduma za Kisheria (LSF) wenye nia ya kuimarisha upatikanaji wa haki, hasa kwa wanawake, wasichana, na jamii zilizotengwa nchini Tanzania.
Ushirikiano huu unathibitisha dhamira yetu ya kukuza maendeleo endelevu na kujenga jamii iliyo na usawakatika upatakanaji wa haki na inayoshiriki kikamilifu katika mfumo wa sheria.
Mradi huu shirikishi unafadhiliwa na Umoja wa Ulaya chini ya mradi unaoitwa “Gender Transformative Action: Breaking the Glass Ceiling” na unalenga kupunguza unyanyasaji wa kijinsia na kuongeza usawa katika upatikanaji wa haki hususani kwa wanawake na wasichana na kuwajengea uwezo wa wasaidizi wa kisheria na watoa msaada wa kisheria kuweza kutoa huduma bora za msaada wa sheria.