Rapa kutoka Marekani Meek Mill ameonyesha nia yake ya kutaka kuwa raia wa Ghan ambapo kwenye tweet yake alitangaza nia yake ya kupata uraia wa Ghana kwa sababu ya ukandamizaji dhidi ya watu weusi huko Marekani unaoendelea.
“Nataka kupata uraia nchini Ghana!!!! Marekani imefanya kuwaangusha watu weusi ikiwa hutafuata amri!” alitweet kwenye chapisho la X mnamo Machi 4, 2024.
Mnamo Desemba 2022, Meek Mill alitumbuiza kwenye jukwaa la Afro Nation na tangu wakati huo amesisitiza nia na mapenzi yake kwa Ghana na hii ilikuwa ni ziara yake ya kwanza kabisa nchini Ghana.
Mwaka huo huo, alitembelea Jubilee House ambako alikutana na kufanya mkutano na Rais Akufo-Addo.
Rapa huyo wa Marekani baadaye alirekodi sehemu za video ya muziki akiwa katika kiti cha serikali jambo ambalo lilizua kelele kutoka kwa wananchi wa Ghana ambao walihoji kwa nini makao ya serikali yanapaswa kudharauliwa hivyo.